- 15,094 viewsDuration: 3:13Habari zaidi zimejitokeza kuhusiana na kifo cha mbunge wa zamani wa Lugari Cyrus Jirongo. Maafisa wa upelelezi wamemhoji mmiliki wa gari aina ya Toyota Probox ambayo ilinaswa kwenye kamera za CCTV ikiwa katika kituo cha mafuta cha Eagol, alikosimama Jirongo muda mfupi kabla ya ajali. Aidha DCI wanaodaiwa kuwa kwenye gari hilo pia wamehojiwa. Jirongo alifariki kwenye ajali baada ya gari lake kugongwa na basi eneo la Karai, Naivasha.