Skip to main content
Skip to main content

Wanahabari waomuomboleza mpiga picha wa KTN Rashid Idi

  • | Citizen TV
    1,728 views
    Duration: 2:07
    Mwanahabari wanaomboleza kifo cha mpiga picha Rashid Idi ambaye alifariki hospitalini Alhamisi. Wanahabari wa runinga za Citizen, KTN na NTV walijumuika na familia ya marehemu katika msikiti wa Masjid Salama Karanja, mtaani Kibra, kabla ya kusafirishwa hadi nyumbani kwao huko Malaba, Bungoma. Rashid alikuwa mpiga picha wa kampuni ya Standard Media Group na alihudumu kwa zaidi ya miongo miwili katika kampuni za Royal Media Services na kisha Standard Group. Wanahabari wenzake wamemtaja kama mtu aliyejituma na kuipenda kazi yake. Ameacha mjane na watoto watatu.