- 225 viewsDuration: 3:34Kiongozi wa kanisa la All Saints Cathedral Nairobi Evans Omollo ametoa wito kwa serikali ifikirie kuongeza tarehe za wanafunzi wa gredi ya kumi kujiunga na shule zao kwa wiki mbili.Kiongozi huyo alisema kanisa limepokea malalamishi mengi kutoka kwa waumini waowanaosema wanahitaji muda zaidi kushughulikia utata unaokumba uteuzi wa shule kwa watoto wao.Baadhi ya wazazi wamelalamika kwamba wanafunzi wengine wa kike wamechaguliwa kujiunga na shule za wavulana na vile vile wavulana kuchaguliwa kujiunga na shule za wasichana, hivyo basi ipo haja ya kuongeza muda ili tatizo hilo lishughulikiwe. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive