Watu sita waliaga dunia leo asubuhi kufuatia ajali ya barabarani katika eneo la Fort Ternan kwenye barabara ya Londiani–Muhoroni katika kaunti ya Kericho. Maafisa wa polisi waliripoti kwamba abiria kadhaa walipata majeraha kwneye ajali hiyo iliyohusisha basi lililokuwa likielekea Busia na wanapokea matibabu. Kwingineko, familia za watu tisa walioangamia katika ajali ya barabarani katika kituo cha Karai huko Naivasha siku ya jumatatu, sasa zinailaumu wizara ya uchukuzi kutokana na ongezeko la ajali za barabarani zinazoshuhudiwa humu nchini. Walikuwa wakizungumza wakati wa utambuzi wa miili ya walioaga dunia.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive