- 2,307 viewsDuration: 5:22Kundi la kwanza la wanafunzi wa gredi ya 10 chini ya mfumo wa mtaala wa umilisi waliripoti katika shule za upili kote nchini kwa ajili ya kuanza kalenda ya masomo ya mwaka 2026. Uchunguzi wa runinga ya KBC katika shule mbalimbali, ulibaini kuwa shughuli ya usajili wa wanafunzi hao iliendelea vyema huku shule nyingi za kutwa zikinakili idadi ndogo ya wanafunzi. Hata hivyo, huku baadhi ya wanafunzi wakifika shuleni, baadhi ya wazazi walikuwa wakitafuta nafasi kwa wanao katika shule mbalimbali za upili. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive