- 3,024 viewsDuration: 2:51Mipasuko ndani ya chama cha ODM imeonekena kuzidi huku kinara wa ODM Oburu Oginga akilazimika kuhutubia mikutano miwili tofauti ya wajumbe wa ODM kaunti ya Kakamega. Hii ni baada ya kundi moja linaloongozwa na mwenyekiti wa ODM kaunti ya Kakamega na gavana wa kaunti hiyo Fernandes Barasa kusisitiza kuwa mkutano wao ndio mkutano halali wa chama huku kundi lingine linalomuunga mkono gavana wa zamani Wycliffe Oparanya nalo likipanga mkutano mwingine eneo la Butere