Skip to main content
Skip to main content

Sarakasi ya kukumbatia mti

  • | Citizen TV
    512 views
    Duration: 1:29
    Mtu mmoja kutoka Kitale aliyeanzisha Jaribio la kukumbatia Mti kwa Saa 120 ili kuonyesha kuwa hana uwezo wa kulipa karo ya binti yake kujiunga na Gredi ya 10 katika Shule ya St Joseph's, amelazimika kukatiza azma yake baada ya kufurushwa na wakazi wa Kitale. Mbunge wa Saboti, Caleb Amisi, aliyefika eneo hilo, alimpa pesa za kulipa karo, lakini jama huyo alisisitiza kuendeleza jaribio hilo. Amisi sasa anaitaka serikali kuweka sheria za kudhibiti majaribio kama haya ili kuepusha kutumiwa vibaya na baadhi ya watu wanaotaka kupata umaarufu kwa njia ya mkato. Baadaye wakazi walimfurusha mwanaume huyo kwa madai kuwa alikuwa na nia fiche, kwani mwanawe tayari alikua amelipiwa karo na Mbunge, na hawakuona haja ya yeye kuendeleza azma hiyo.