Skip to main content
Skip to main content

Wanafunzi wameondolewa kwenye madarasa hatari Vihiga

  • | Citizen TV
    196 views
    Duration: 2:18
    Shughuli za masomo zimetatizika katika shule ya msingi ya Bahati ADC eneo bunge la Hamisi, Kaunti ya Vihiga baada ya Jumba la ghorofa moja kuonyesha dalili za kuporomoka. Hali hiyo imelazimu usimamizi wa shule kuwahamisha wanafunzi hadi eneo mbadala.Kulingana na baadhi wa wazazi katika shule hiyo, darasa hilo lilijengwa kwa kutozingatia kanuni za ujenzi, hali ambayo imehatarisha maisha ya wanafunzi. Maafisa kutoka Idara ya ujenzi Kaunti ya Vihiga walifika katika shule hiyo na kukagua jengo hilo kabla ya wanafunzi kuondolewa.