Viongozi wa muungano wa kutetea walimu, KUPPET inazidi kushinikiza serikali kupiga jeki zaidi masomo ya wanafunzi wa gredi ya 10 kwani licha ya wengi kufika shule masomo yangali kuanza rasmi wakitaja changamoto nyingine inayokodolea macho walimu wa CBE ni ukosefu wa walimu wa masomo kadhaa.
Wakizungumza mjini Kisii, viongozi hao wa Kuppet wameongeza kuwa ukosefu wa vitabu katika shule mbalimbali za gredi ya 10 huenda ukasababisha kujikokota kwa mtaala wa gredi ya 10 kwani mpaka sasa kuna baadhi ya shule zimepokea tu vitabu viwili kutoka wizara ya Elimu. Aidha wameomba wazazi kutekeleza wajibu wao wa kuhakikisha wanao wanasoma katika mazingira ya kuridhisha serikali ikitekeleza majukumu yake.