- 7,067 viewsDuration: 3:38Kwa kawaida, vituo vya polisi hutembelewa na wananchi wanaotaka kuripoti uhalifu au kuwasilisha malalamishi mbalimbali kabla ya kesi kufikishwa mahakamani. Lakini siku ya Jumanne, hali ilikuwa tofauti katika kituo cha polisi cha Kapsabet. Sandra Cheptoo alisafiri umbali wa zaidi ya kilometa kumi kufika katika kituo hicho, si kwa ajili ya kuripoti uhalifu, bali kuwasilisha taarifa ya ukosefu wa karo ya shule. Sandra, ambaye alifanya vyema katika mtihani wa KJSEA, alipata barua ya kujiunga na Shule ya Upili ya Wasichana ya Ndalat, lakini changamoto ya karo imekuwa kikwazo kikubwa katika kutimiza ndoto yake ya kuendelea na masomo. Mwanahabari wetu Daniel Korir na kina cha taarifa hiyo.