Waajiri sasa wanapewa changamoto ya kuhakikisha kuwa wafanyikazi wao wanafanya kazi katika mazingira ambayo yanaleta furaha. Taasisi ya Makatibu Walioidhinishwa nchini sasa inashirikiana na shirika la furaha la kenya ili kujumuisha masuala ya furaha katika mtaala wao na pia kutuza taasisi zinazokuza furaha kazini. Taasisi hiyo ya Makatibu ni muhimu katika kutoa mafunzo kwa wasimamizi wa ngazi za juu katika taasisi mbalimbali nchini na inaendesha mpango wa tuzo chini ya mabingwa wa tuzo za utawala na hivyo basi, ushirikiano huo utawezesha taasisi ambazo zimeanzisha furaha kama kigezo cha kuthaminiwa.