- 629 viewsDuration: 5:57Mahakama Kuu nchini Kenya imetupilia mbali ombi la kutaka kulipwa fidia kwa waathiriwa wa mlipuko wa bomu wa mwaka 1998 uliotokea jijini Nairobi, ikiamua kuwa waombaji walishindwa kuthibitisha kuwa serikali ilipuuza wajibu wake wa kuzuia shambulio hilo. Katika hukumu iliyotolewa Jumatano, Jaji Lawrence Mugambi aliamua kwamba ombi hilo, lililowasilishwa mwaka wa 2021, halina umuhimu na halikuthibitisha uwajibikaji kwa upande wa serikali. #DiraYaDuniaTV