lShughuli za masomo katika Shule ya Msingi ya Meswo huko Emgwen, Kaunti ya Nandi, zilisitishwa baada ya wazazi wenye ghadabu kufunga shule hiyo na kumfurusha mwalimu mkuu.
Maafisa wa usalama na wasimamizi wa elimu walilazimika kuingilia kati ili kutuliza ghasia zilizozuka. Kwa sasa, naibu mwalimu mkuu amechukua usukani wa muda huku mwalimu mkuu ambaye amehudumu shuleni humo kwa miaka saba, akiagizwa kuripoti katika ofisi za elimu mjini Kapsabet. Wazazi wanadai kuwa mwalimu huyo amekuwa akitumia mamlaka yake vibaya.