Skip to main content
Skip to main content

Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro akosoa jinsi hisa za Safaricom na KPC zinauzwa

  • | Citizen TV
    617 views
    Duration: 2:01
    Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro anasisitiza kuwa uuzaji wa asilimia 15 ya hisa za kampuni ya safaricom zinazomilikiwa na serikali zitawakosesha wakenya nafasi ya kupata faida zaidi. Nyoro anasema kuwa uuzaji wa hisa hizo kwa shilingi bilioni 204 kunadunisha thamani ya kampuni hiyo ilhali serikali inaweza kupata shilingi bilioni 150 zaidi iwapo ingewekwa wazi kwa kampuni za kimataifa. Akizungumza kwenye mkutano na wanasiasa chipukizi mjini Embu,Nyoro amesema kuw akuna njama ya maafisa wakuu serikalini kununua hisa hizo kwa bei duni. aidha nyoro amesema kuwa sakata hiyo hiyo ndiyo inayofanyika kwenye uuzaji wa hisa za kampuni ya kenya pipeline ambazo watu wachache wenye ushawishi wametengewa asilimia 20 hadi 25 ya hisa hizo.