- 1,064 viewsDuration: 2:06Watu wawili ameuawa huku wengine watatu wakijeruhiwa vibaya baada ya kushambuliwa kwa visu katika mtaa wa Matisi na Forkland, viungani mwa mji wa Kitale, kaunti ya Trans Nzoia. Tukio hilo limezua hofu miongoni mwa wakazi wa eneo hilo. Kwa mujibu wa familia ya marehemu, Fredrick Subai alikumbana na mauti alipokuwa akirejea nyumbani kutoka katika Kanisa la St Kizito Matisi saa moja jioni. Inadaiwa kuwa genge hilo la wahalifu liliwashambulia waathiriwa kabla ya kutoroka na simu zao. Wakazi wa maeneo hayo sasa wanaitaka serikali ya kaunti pamoja na vyombo vya usalama kuongeza doria ili kudhibiti visa vya uhalifu.