- 4,427 viewsDuration: 1:15Waraka umewasilishwa kushinikiza kuondolewa kwa Isaac Ruto kama mwanachama wa tume ya mahakama JSC, kwa tuhuma za kuhujumu uhuru na utendakazi wa tume hiyo. Waraka huo umewasilishwa na kupokewa rasmi kwa karani wa bunge. Shinikizo la kumwondoa Ruto limejiri huku aliyekuwa naibu mwenyekiti wa JSC Macharia Njeru, akimwandikia waraka jaji mkuu Martha Koome ambaye pia ni mwenyekiti wa JSC, kumshtumu Ruto kwa kujihusisha na shughuli za kisiasa za chama cha UDA. Njeru amesema kuwa ya Ruto inakiuka katiba na kanuni za nidhamu za JSC na kuonya kuwa inahujumu uhuru wa idara ya mahakama.