Huku serikali ikipendekezea vyama vya ushirika vya humu nchini kupunguza riba wanazotoza wanachama wanapochukua mikopo hadi asilimia ya tisa au chini, Mashirika haya sasa yanaonya kuwa hatua hiyo inatishia kupunguza mgao wa kila mwaka kwa wanachama na pia kuhatarisha mashirika hayo.
Katibu wa vyama vya ushirika Patrick Kilemi, ameonya vyama vya ushirika dhidi ya kuhujumu akiba za wakenya na kuwataka kutoa mikopo kwa wanachama wanapohitaji. aidha kilemi ameonya mashirika hayo dhidi ya ubadhirifu wa pesa za wawekezaji.