Skip to main content
Skip to main content

Chakula cha msaada Marsabit

  • | Citizen TV
    236 views
    Duration: 1:41
    Maeneo ya Kaskazini mwa nchi yanakabiliwa na mzozo mkubwa wa kibinadamu huku ukame wa muda mrefu ukiendelea kusukuma familia nyingi kwenye njaa na utapiamlo. Katika kaunti za Marsabit na Mandera, maelfu ya familia zilizo hatarini na zinapata ugumu wa kupata mlo kufuatia kukosekana kwa mvua, kukauka kwa vyanzo vya maji, na kuangamia kwa mifugo.Wakazi hao wamesambaziwa Magunia 1,115 ya msaada wa chakula. Katika kaunti ya Marsabit, familia 450 katika eneo la Korr zilinufaika, huku familia 650 katika maeneo tisa ya Mandera Mashariki pia zikipokea msaada huo.