Skip to main content
Skip to main content

Bima ya afya ya SHA italipia upasuaji 36 pekee, waziri Duale asema

  • | Citizen TV
    629 views
    Duration: 3:06
    Bima ya afya ya SHA sasa itakuwa ikilipia huduma za matibabu za upasuaji wa aina 36 pekee ambazo hazipatikani hapa nchini. Hiyo inamaana kuwa SHA sasa haitalipia kila aina ya matibabu ambayo mkenya aliyesajiliwa chini ya SHA atakwenda kutafuta ughaibuni. Jopo la ushauri wa manufaa ya matibabu Limesema huduma hizo zitalipiwa kikamilifu huku waziri wa afya Aden Duale akisema hatua hiyo inanuiwa kuzuia wakenya kutafuta matibabu nje ya nchi pamoja na kukabiliana na ufisadi