Skip to main content
Skip to main content

IPOA yaanzisha uchunguzi wa polisi kufuatia shambulizi kanisa Nyeri

  • | Citizen TV
    1,569 views
    Duration: 2:46
    Mamlaka ya kuchunguza utendakazi wa maafisa wa polisi IPOA na kitengo cha kuwachunguza maafisa wa polisi vimeanzisha uchunguzi wa kubaini iwapo maafisa wa polisi walihusika kwenye shambulizi la kanisa la ACK Witima huko Nyeri. Ibada hiyo ilikuwa ikihudhuriwa na kinara wa DCP Rigathi Gachagua jumapili iliyopita. Mratibu wa eneo la kati Joshua Nkanatha, amewarai maafisa wa polisi na wale wa utawala kutojihusisha na ghasia na kuwataka kuzingatia kanuni zinazoongoza utendakazi wao, kama Kamau Mwangi anavyoarifu.