- 320 viewsDuration: 2:24Runinga ya Citizen imetuzwa kwa kudumisha chapa bora kwa matangazo na vipindi nchini Kenya na kanda ya Africa Mashariki. Katika hafla ya uzinduzi ya nakala ya 9 ya ‘the Superbrands East Africa book” Runinga ya citizen ilitamba kwa udhibiti wa uhalisia ya vipindi na matangazo huku ikitambuliwa kutamba katika Nyanja ya utangazaji. Hafla hiyo ilihudhuriwa na wafanyakazi wa kampuni ya Royal Media Services ikiongozwa na mkuu katika kitengo cha mauzo Carol Washira.