- 291 viewsDuration: 1:57Swala la umasikini limetajwa kama miongoni mwa changamoto zinazokumba wazazi wengi katika eneobunge la mlima Elgon kaunti ya bungoma hatua ambayo imechangia baadhi ya watoto kutohudhuria masomo. Wazazi wa wadi ya kapkateny wanasema mara nyingi wana wao hukosa kuhudhuria masomo kutokana na ukosefu wa mahitaji ya kimsingi zikiwemo sare rasmi za shule hatua ambayo inalemaza shughuli za masomo eneo hilo