Skip to main content
Skip to main content

Wanafunzi wa shule ya Our Lady of Mercy mjini Busia wasaidiwa

  • | Citizen TV
    388 views
    Duration: 2:05
    Huku machifu na makatibu wakuu serikalini wakitwikwa jukumu la kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wa gredi ya kumi wanajiunga na sekondari za juu, wanafunzi wasiojiweza wamelengwa katika shughuli ya usambazaji wa msaada wa chakula kutoka kwa serikali kuu. Akizungumza wakati wa kusambaza chakula hicho katika shule ya upili ya wasichana ya Our Lady of Mercy mjini Busia, katibu wa mipango Boniface Makoha amesema kuwa lengo lao kuu ni kukabili changamoto zote ili kuhakikisha asilimia 100 ya wanafunzi wameenda shuleni na kuboresha matokeo...