Chama cha Walimu KUPPET kimeibua wasiwasi kuhusu uuteuzi wa wanafunzi wa gredi ya 10 chini ya mtaala mpya, kikionya kuwa hatua hiyo inaweza kusababisha kutoweka kwa shule za C4. Akizungumza mwishoni mwa wiki wakati wa uchaguzi wa tawi la KUPPET Kaunti ya Baringo, Mwenyekiti wa Muungano huo, Omboko Milemba, alisema kuna haja kwa Wizara ya Elimu kuratibu upya mchakato wa upangaji wa wanafunzi. Alibainisha kuwa shule za C4 kwa kiasi kikubwa huhudumia wanafunzi kutoka familia maskini na zinaweza kuathirika pakubwa na mpangilio mpya wa uteuzi.