- 140 viewsDuration: 3:43Wagonjwa wa saratani katika hospitali ya kitaifa ya kenyatta wameeleza masaibu yao kufuatia kukatika mara kwa mara kwa mfumo unaotoa huduma kupitia bima ya sha. Wagonjwa pamoja na walezi wao wamesema hali hii imewalazimu kusubiri hadi siku tatu kupata matibabu. Na huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya saratani, wagonjwa hao wanaitaka serikali kutekeleza maagizo ya rais ya kuongeza fedha za sha kwa wagonjwa wa saratani kutoka shilingi laki tano hadi shilingi laki nane