Vifo Mpakani": Africa Eye inachunguza moja ya siku mbaya zaidi mipakani huko Ulaya

  • | BBC Swahili
    4,533 views
    Mnamo Juni 2022, video za kutisha zilianza kusambazwa mtandaoni, zikionyesha mapigano makali kati ya Wahamiaji wa Kiafrika na walinzi wa mpaka wa Morocco. Walirekodiwa katika sehemu ambayo Morocco inakutana na Uhispania - lango la kuingia Ulaya na kuonyesha miili ya Wahamiaji wa Afrika wakitupwa chini, kupigwa na kupondwa pondwa. Watu ishirini na nne walifariki katika tukio hilo na wengine wengi bado hawajulikani walipo. Africa Eye imethibitisha makumi ya video, zenye ushuhuda uliokusanywa kutoka kwa walionusurika na kupata nafasi adimu ya kufika barabara ya mpakani na kuandaa tarifa ya uchunguzi wa kina zaidi wa mkasa huo na kuuuliza je haikuwezeana kuzuilika? #bbcswahili #africaeye #uhamiaji