- 11,728 viewsDuration: 1:56China imevutia macho ya dunia baada ya kuonyesha rasmi kwa mara ya kwanza ndege yake mpya ya kivita J-20A pamoja na J-20S yenye viti viwili, katika maadhimisho ya miaka 15 tangu J-20 ifanye safari yake ya kwanza angani. Kwa mujibu wa wataalamu wa kijeshi, J-20A si maboresho ya kawaida bali ni mabadiliko makubwa ya kimkakati yanayolenga kuimarisha uwezo wa anga wa China, hasa katika eneo la Asia-Pasifiki. Maboresho hayo yanahusisha muundo, teknolojia na uwezo wa kivita, hatua inayoweza kubadilisha mizani ya nguvu za kijeshi duniani. Katika video hii, mwandishi wa BBC @frankmavura anabainisha baadhi ya sifa kuu za ndege hiyo mpya ya kivita. #bbcswahili #China #ndegeyakijeshi Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw