- 436 viewsDuration: 1:41Wanaharakati wa Afya waongeza juhudi za kupambana na saratani kupitia kampeni ya nyumba kwa nyumba katika eneo la Watamu, Kaunti ya Kilifi, wakilenga kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kugundua mapema ugonjwa huo hatari. Wanaharakati hao, ambao baadhi yao pia ni waathiriwa wa ugonjwa wa saratani, wametembelea makazi ya wanavijiji wakitoa elimu kuhusu dalili za mapema za saratani na umuhimu wa kupima hali ya afya mara kwa mara.