- 101 viewsDuration: 1:12Siku moja baada ya muungano wa wauguzi kuibua madai ya wauguzi bandia wanaohudumu kwenye hospitali mbalimbali katika kaunti ya Nyamira, Waziri wa afya katika kaunti hiyo Dkt. Donald Mogoi amejitokeza na kupinga vikali madai hayo. Akizungumza na wanahabari katika hospitali ya rufaa ya Nyamira Mogoi amesema kabla kuajiri mhudumu yeyote wa afya, idara yake hupiga msasa stakabadhi na kuhakikisha kila mhudumu ana leseni ya kuhudumu kisheria.