- 407 viewsDuration: 56sRaia watano wa Ethiopia wamefikishwa katika mahakama ya Garissa kwa kosa la kuwa nchini kinyume cha sheria. Watano hao walikamatwa mnamo tarehe 30 Januari mwaka huu katika kivukio cha mto Tana wakitembea kwa miguu kuelekea mji wa Madogo ili kukwepa upekuzi wa maafisa wa usalama. Washukiwa hao walikiri mashtaka hayo na kuachiliwa kwa faini ya shilingi elfu kumi kila mmoja ama kifungo cha mwezi moja.