- 17,259 viewsDuration: 2:45Kundi la ODM linaloongozwa na katibu mkuu Edwin Sifuna limesisitiza kuwa halitaruhusu chama hicho kubuni muungano na chama cha UDA kuunga mkono urais wa Rais William Ruto kwenye uchaguzi mkuu ujao. Wakiendeleza mikutano na wananchi kaunti ya Busia, viongozi hao wameshikilia kuwa wako tayari kuchukua usukani wa chama na kuwa ni lazima ODM iwe na mgombea wa urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.