- 85 viewsChama cha United Green Movement UGM kimendeleza kampeni zake za kuhamasisha wakenya kujisajili kama wapiga kura katika kaunti ya Garissa. Jaji Mstaafu David Maraga akituma fursa kupitia chama chake cha UGM kuhamasisha vijana kujisajili zaidi kama wapiga kura. Maraga akiishtumu tume ya uchaguzi ya IEBC kwa kukosa kutumia fursa iliyo wazi kuandikisha wenyeji kama wapiga kura. Maraga pia akiitaka IEBC kuzuru maeneo ya mashinani na sehemu za ibada na kuwasajili wote waliohitimu kupiga kura. Pia amepuuza tetesi kuwa ni kibaraka wa mrengo fulani kwenye azma yake ya kuwania urais mwakani.