- 26,601 viewsDuration: 3:22Siku moja baada ya runinga ya citizen kuangazia taarifa kuhusu visa vya uhalifu baadhi ya maeneo nchini, waathiriwa zaidi wamejitokeza na kuelezea masaibu yao mikononi mwa wahalifu waliojihami kwa silaha hatari. Watu saba wanauguza majeraha baada ya kuvamiwa na genge la watu sita katika duka la kuuzia mvinyo katika barabara ya muhuri, kiambu wiki jana. Kulingana na waathiriwa, wahalifu waliojihami kwa bastola walibeba mmoja wao na kumtupa katika mtaa wa juja alikookolewa na maafisa wa polisi wa kikuyu saa tatu baadaye