Malumbano kati ya magavana na maseneta yanaonekana kuchacha huku maseneta wakiwatuhumu magavana kwa kutumia ujanja kuepuka kuwajibikia matumizi ya pesa za umma. Mwenyekiti wa kamati ya seneti kuhusu uhasibu wa fedha za umma kwenye kaunti, Moses Kajwang na mwenzake wa kamati ya uwekezaji katika kaunti, Godfrey Osotsi, kwenye mahojiano na shirika la utangazaji humu nchini, KBC walionya kuwa magavana wanaokaidi mwaliko wa kufika mbele ya kamati za bunge hilo watawajibishwa na mgao wa bajeti kwa kaunti zao kusitishwa.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive