Skip to main content
Skip to main content

SHA haitagharamia matibabu nje ya nchi

  • | KBC Video
    259 views
    Duration: 2:56
    Wakenya wanaotafuta matibabu nje ya nchi sasa watalazimika kugharamia huduma hizo licha ya kuchangia kwenye hazina ya bima ya afya ya jamii SHIF. Afisa mkuu mtendaji wa halmashauri ya afya ya jamii SHA Mercy Mwangangi aliyefika mbele ya kamati ya bunge, alisema halmashauri hiyo ingali kutia saini kandarasi na hospitali za kigeni kama inavyohitajika kisheria, na hivyo haiwezi kugharamia matibabu nje ya nchi. Mwangangi hata hivyo aliwahakikishia wakenya kuwa utaratibu wa kuidhinisha hospitali za kigeni utakamilika kufikia mwisho wa mwezi ujao na orodha ya hospitali hizo kuwekwa hadharani. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive