Dalali aliyebomoa jumba mtaani westlands afikishwa mahakamani

  • | Citizen TV
    2,402 views

    Mahakama kuu jijini Nairobi imemtaka wakili na dalali katika kesi ya ubomozi wa jumba la Niraj Shah na mkewe Avani Shah katika mtaa wa Westlands waeleze kupitia hatikiapo sababu ya kutekeleza ubomozi huo bila idhini ya mahakama jaji Oscar Angote amesema mahakama imebainisha kuwa amri ya mahakama kuhusu jumba hilo la shilingi milioni 80 haikumruhusu dalali kubomoa nyumba hiyo. Jaji Angote ameamuru maelezo zaidi kutolewa kabla ya ijumaa wiki hii, huku kesi hiyo ikitarajiwa kusikizwa siku ya jumatatu. Upande wa mashtaka uliomba siku kumi na nne kumzuia dalali aliyehusika na ubomozi huo zachary baraza. Uamuzi kuhusu iwapo baraza ataachiliwa kwa dhamana au la utatolewa kesho.