Jiji la Nairobi lilipambwa kwa rangi nyekundu hii leo, huku wakazi wakiungana na ulimwengu kuadhimisha siku ya wapendanao almaarufu ‘Valentine’s Day’. Biashara ya uuzaji wa maua na vifurushi vya zawadi ilinoga, huku wateja wakinunua maua mekundu, mvinyo na chokoleti miongoni mwa bidhaa nyingine. Hata hivyo wafanyibiashara walisema kiwango cha biashara kilikuwa cha chini ikilinganishwa na miaka ya awali hali ambayo walisema inatokana na hali ngumu ya kiuchumi.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive