- 169 viewsDuration: 1:23Viongozi wa chama cha kutetea maslahi ya walimu wa sekondari na vyuo vya kadri KUPPET eneo la Bungoma kaskazini wameelezea mahangaiko ambayo walimu wanakumbana nayo wanapotafuta huduma za matibabu kupitia bima ya SHA. Viongozi hao wameitaka serikali kuwajibikia suala hilo kwa upesi ili walimu wapate afueni kutokana na mahangaiko wanayopitia kila kuchao. Wakizungumza katika shule ya sekondari ya wavulana ya St.Patrick's Naitiri, pia wamesisitiza haja ya sekondari msingi kupewa uhuru wa kujisimamia.