- 3,434 viewsDuration: 4:03Watu saba walijeruhiwa baada ya polisi kurusha vitoa machozi kwenye mkutano wa kisiasa wa mrengo wa ODM unaoongozwa na katibu mkuu Edwin Sifuna eneo la Kitengela kaunti ya Kajiado hapo jana. Mkutano huo ulitatizwa na wingu la vitoa machozi huku wanasiasa waliozungumza wakielezea uungaji mkono wao kwa Sifuna kusalia Katibu mkuu. Aidha, waliendelea kurusha makali kwa wale wanasema wameuza na kuvuruga chama cha ODM.