- 183 viewsDuration: 2:03Wakazi 2,500, wakiwemo wazee na vijana kutoka eneo la Engwen katika Kaunti ya Nandi, wamepata afueni baada ya kunufaika na kambi ya matibabu bila malipo na kampeni ya uhamasishaji dhidi ya utumiaji wa dawa za kulevya. Kambi hiyo ya matibabu, iliyoandaliwa na kundi la wasamaria wema pamoja na wanafunzi wa utabibu kati chuo kikuu cha Moi, iliwaleta pamoja wataalamu wa afya ambao walitoa huduma za kipekee, ushauri wa kitaalamu, na dawa kwa wagonjwa mbalimbali.