- 326 viewsDuration: 1:25Mbunge wa Eldas, Adan Keynan, ametoa wito wa usawa katika utoaji wa huduma za serikali, akisema wakazi wa Maeneo Kame wanastahili haki na fursa sawa na Wakenya wengine kote nchini. Akizungumza katika eneo la Eldas, mbunge huyo alisema kwa muda mrefu jamii za Kaskazini mwa Kenya zimekumbwa na changamoto za kutengwa kimaendeleo, lakini akabainisha kuwa hali hiyo inaendelea kubadilika.