Utata unanukia kwenye mpaka wa kaunti za Busia na Bungoma katika eneo la Changara Teso kaskazini, baada ya mbunge wa Sirisia John Waluke kudai kuwa eneo hilo liko katika kaunti ya Bungoma wala si Busia.
Madai ya mbunge huyo yamewaghadhabisha baadhi ya viongozi wa kaunti ya Busia wanaoitaka tume ya ncic kuingilia kati ili kuepuka kuzuka kwa uhasama miongoni mwa wakazi wa kaunti hizo mbili zinazopakana. Kwa mujibu wa viongozi hao hapo jana, wamelazimika mara kadhaa kuzuia Changara kuwa katika eneo bunge la Sirisia katika kaunti ya Bungoma ili kisheria na katika stakabadhi za serikali itambulike kuwa sehemu ya eneo bunge la Teso kaskazini, utata huo sasa unahofiwa kuwa huenda ukazua uhasama wa kikabila kwa jamii zinazoshi katika eneo hilo, viongozi wakishindwa kuendeleza eneo hilo.