Skip to main content
Skip to main content

Mzozo wa wafanyikazi wa kaunti watatiza uchaguzi wa kitaifa

  • | Citizen TV
    406 views
    Duration: 1:52
    Uchaguzi wa kitaifa wa muungano wa chama cha wafanyikazi wa serikali za Kaunti nchini ulioratibiwa kufanywa jana Katika kaunti ya Nakuru, uliahirishwa baada ya kundi linaloongozwa na anayewania nafasi ya katibu Mkuu wa muungano huo Vescah Kagongo kuelekea mahakani mjini Machakos na kuomba Mahakama kusitisha uchaguzi huo Kwa misingi ya udanganyifu wa uchaguzi huo. Wakihutubia wanahabari Jana Jioni, punde baada ya maafisa wa polisi kufaulu kusimamisha uchaguzi huo ambao tayari ulikuwa umeanza, Vescah Kagongo alisema Katibu Mkuu wa sasa alibadisha Sheria za uchaguzi wa muungano huo na kufanya vigumu wawaniaji wengine kuwania, hali hiyo ikimpa nafasi Katibu anaehudumu kuwania pekee yake, kesi iliyowasilishwa mahakamani itasikizwa mwezi wa tatu.