Skip to main content
Skip to main content

Wazee wa Abagusii wairai jamii kuendeleza amani kote nchini

  • | Citizen TV
    245 views
    Duration: 2:09
    Baraza la Kitaifa la Wazee wa Abagusii limewarai wakaazi wa Abagusii kuendeleza mshikamano, amani na maadili mema ili kuimarisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi, huku wakiwataka viongozi wa kisiasa na kijamii kuunganisha jamii tofauti badala ya kutoa matamshi yanayoweza kuchochea ukabila na migawanyiko. Wakizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa ofisi ya Abagusii mjini Kitale katika Kaunti ya Trans Nzoia, wazee hao wakiongozwa na James Matundura wamesema ofisi hiyo mpya itatumika kuratibu masuala ya kijamii, kusaidia katika utatuzi wa migogoro na kuimarisha maadili ya kitamaduni. Walisema pia kuwa ofisi hiyo itakuza ushirikiano kati ya wazee na vijana, hatua ambayo itachangia katika kulea kizazi chenye nidhamu na maono.