Skip to main content
Skip to main content

Baadhi ya viongozi wa ODM wasisitiza chama hicho kipewe wadhifa wa naibu rais

  • | Citizen TV
    6,936 views
    Duration: 1:50
    Baadhi ya viongozi wa Chama cha ODM na UDA wanaomuunga mkono Rais William Ruto kuongoza kwa muhula wa pili wameendeleza mvutano unaoshuhudiwa kwa sasa kuafuatia matamshi ya chama cha ODM kutaka wadhifa wa naibu rais. Wakizungumza eneo bunge la Narok Kusini walipozindua rasmi darasa la shule ya upili ya Ilkirein-Loita mbali na kuzindua mradi wa kujenga na kurekebisha mabwawa ya maji vijijini huko wamesisitiza kuwa itawezekana kwa Rais Ruto kusalia kwa kiti chake lakini ni sharti ODM ipewe wadhifa wa naibu rais. Mwenyekiti wa kamati ya bajeti na uhasibu katika bunge la Kitaifa ambaye pia ni mbunge wa Alego Usonga Samwel Atandi pia amewakosoa viongozi wa upinzani kwa kuendeleza madai ya ufisadi.