Skip to main content
Skip to main content

Kundi la asasi za kiraia lawakosoa magavana kwa kukaidi usimamizi wa katiba

  • | Citizen TV
    250 views
    Duration: 1:45
    Kundi la Asasi za Kiraia za ugatuzi nchini limeibua tahadhari kuhusu kile limetaja kama juhudi za kimfumo za kudhoofisha ugatuzi, likiwashutumu magavana kwa kukaidi usimamizi wa kikatiba na vile vile tuhuma za ufisadi ndani ya mifumo ya uwajibikaji. kundi hilo limesisitiza kuwa jukumu la Seneti kutathmini matumizi ya fedha za kaunti ni wajibu wa kikatiba, si hisani, na kueleza wasiwasi wake kufuatia ripoti kuwa magavana wameazimia kususia vikao vya Kamati ya Seneti . kundi hilo sasa linaitaka idara ya ujasusu - DCI na Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi - EACC kufanya uchunguzi na kuchukua hatua kali dhidi ya watakaopatikana kuhusika kwa kutoa au kupokea hongo.