Chuo cha Mafunzo ya Ualimu cha Abardare katika eneo mbunge la Ndaragwa kaunti ya Nyandarua kimenufaika na mradi wa ujenzi wa bweni la wanafunzi la ghorofa tano na lenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 680.
Mradi huu wa thamani ya takriban Shilingi milioni 346, utatekelezwa kupitia Idara ya Serikali ya Makazi na Maendeleo ya Miji kwa ushirikiano na hazina ya maeneo bunge ya Ndaragwa NG-CDF na unanuiwa kufanikisha malazi bora katika taasisi hii ya mafunzo ya umma kama sehemu ya Mpango wa Makazi ya bei nafuu wa serikali. Baada ya kukamilika, Bweni hili jipya itafungua njia kwa mradi mwingine kama huo ambao utasaidia kushughulikia changamoto za sehemu za kulala kwa idadi ya wanafunzi inayoongezeka