Wakulima katika eneo la chini la Mashariki wamehimizwa kutumia mbegu iliyoidhinishwa ili kuongeza nafasi ya mavuno bora.
Akizungumza huko Machakos wakati wa kongamano la kutoa hamasisho kwa wakulima kabla ya msimu wa upanzi, mkurugenzi mkuu wa Bayer East Africa John Kanyingi alisema hali ya hewa isiyotabirika katika eneo la Ukambani inahitaji matumizi ya mbegu iliyoidhinishwa na ambayo inaweza kuhimili kiasi kidogo cha mvua.
Mkuu wa kitengo cha biashara cha Wakulima Wadogo barani Afrika, Everlyn Musyoka, amesema wanatoa nafasi kwa wakulima kupata mbegu halisi na ambayo itasaidia kutoa mazao bora.