Maafisa wa Mamlaka ya Kitaifa ya Kupambana na Matumizi ya Pombe na Dawa za Kulevya NACADA wamesema wataanza kutekeleza sheria mpya ya mwaka 2025 inayolenga kuwanyang’anya mali watu waliopata utajiri kupitia ulanguzi na uuzaji wa mihadarati pamoja na pombe haramu.
Hatua hiyo imewadia baada ya kukamilika kwa kampeni ya wiki moja ya kuhamasisha umma dhidi ya matumizi ya pombe kwenye chupa za plastiki katika kijiji cha Mugundoi, eneo bunge la Nandi Hills, Kaunti ya Nandi. Mshirikishi wa NACADA katika kaunti za Nandi na Uasin Gishu, Calvin Olula, amesema mamlaka hiyo haitavumilia tena uuzaji au usambazaji wa pombe zisizokidhi viwango vinavyotakiwa, akionya kuwa watakaopatikana na hatia watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kunyang’anywa mali.