- 186 viewsDuration: 1:06Waumini kutoka Kanisa katoliki la St Ann Muthure wameungana na wenzao kote ulimwenguni kwa mwanzo wa kipindi cha Kwaresima kupitia maadhimisho ya Jumatano ya Majivu. Padre Simon Peter Ndungu aliyeongoza ibada hiyo aliwahimiza waumini kutafakari, kutubu na kuimarisha maisha yao ya kiroho katika kipindi hiki cha siku 40 kuelekea Pasaka.